
Baada
ya wapenzi wa muziki Tanzania kusubiri kwa muda mrefu sasa wamepata
nafasi ya kujiburudisha na ngoma mpya kutoka kwa Alikiba. Tarehe 25
Julai, 2014 Alikiba ameachia single mpya iitwazo “Mwana” . Alikiba
anajulikana ndani na nje ya Tanzania kwa hit zake kama Cinderella,
Mapenzi yanarun dunia, Single boy, na Dushelele. Cinderela ndiyo wimbo
ambao mpaka sasa umeweka rekodi ya kuuza copy nyingi katika Afrika
Mashariki mwaka 2008. Mwaka 2012 Alikiba alishinda tuzo ya best Rhumba/
Zouk na wimbo wake wa “Dushelele” katika tuzo za Kilimanjaro Tanzania
Music Awards. Alikiba anajulikana kwa uwezo wake mkubwa wa kuimba na
utunzi wa nyimbo pamoja na kuwa mburudishaji mkali sana katika show zake
za live na mpaka sasa ametembea nchi nyingi sana duniani kuburudisha
wapenzi wa muziki.
0 maoni:
Post a Comment
to maoni n ushauri wako kuhusu post zetu