Huwezi kuchoka kumsifia hata siku moja utakapobahatika kukutana nae ni mrefu mwenye umbo la asili lililoneemeshwa na makalio ya kihasi yaliyopewa hips za nguvu zilizokubali vazi lolote hata kama angevaa gunia...
Macho yake yaliyoonekana kama yanadondoka hasa anapokuangalia kutokana na ukubwa wake na jinsi yalivyolegea yalizidi kuupamba uso wake wa duara wenye kope nyingi zisizo za bandia na lips ndogo ambazo muda wote zimelowa
Mwenye tabasam lenye kushawishi na wew kutabasamu kama ungefanikiwa kugonganisha nae macho...
Umaskini wa familia yao ulisababisha wanaume washindwe kuuina uzuri huo kwa harakaharaka lakini mimi umakini wangu wa kuchunguza mke bora ulinifanya nione uzuri huo...
Mavazi ya khanga ndio aliopendelea kutokana na kushindwa kugharamia mavazi ya kimitindo laki bado alipemdeza kwani khanga zilifanya maumbile yake kwa nyuma kutikisika akiwa anatembea...
Rangi yake ya chocolate ambapo wenye rangi hii napenda kuwaitwa black beuties kwani ndio rangi ninayoipenda kwa mwanamke lakini yakwake ilikua kidogo imechakaa kutokana na dhiki japo bado ilionesha urembo wake...
.......................................................
Ilikua jioni ya furaha kwangu kukanyaga tena ardhi ya Afrika nchi ya Tanzania nchi ambayo niliipenda kutoka moyoni kwa baraka tulizojaaliwa japo kulikua na kasoro ndogo kwa baadhi ya viongozi wake...
Katika uwanja wa ndege wa kimayaifa wa mwl julius kambarage nyerere furaha yangu ilizidi baada ya kumuona rafiki yangu kipenzi Said akiwa amekuja kunipokea...
Said tulifahamiana kuanzia primary school tukatengana o level lakini tukaja kutana tena katika shule ya Umbwe iliopo kilimanjaro na baadae kuendelea pamoja elimu ya chuo mpaka sasa tukifanya kazi wote kwenye kampuni ya Sayusfa import
Hibyo urafiki wetu ulikuwa wa kihistoria kwani hata pale kampuni iliponipa nafasi ya kwenda kusoma nchini uingereza tuliendelea kuwasiliana..
Kwa furaha aliyonayo alinipitisha kwake na kumuaga mkewe kisha tukaenda kula bata olympic hotel
Mwenzangu alikua tayar ameshaoa na anamtoto mmoja alieitwa Layla
Nilitamani sana silu moja na mimi niitwe baba kama ambavyo yeye aliitwa ..
Nilifika kazini siku iliyofuata na kuanza kazi mara moja kama afisa manunuzi wa kampuny...
Hakika niliingizia kampuny mapato mengi kutokana na umahili wangu katika kazi mpaka kampuny kuamua kunilipa mshahara ambao mimi niliitaji..
Hali hiyo ilinifanya nipate tamaa ya kuanzisha kampuny yangu nikiamini nitafanya vizuri zaidi
Miaka miwili baadae ndoto zangu zilitimia kwa kuanzisha kampuni yangu ya usambazaji bidhaa na kujitoa katika mikono ya kuajiliwa...
Niliamua kumchukua Said na kumpa umeneja katika kampuny yangu
Kutokana umahili wa kazi kutoka kwa wafanya kazi niliowachukua moja kwa moja kutoka vyuoni nilijikuta nakua kwa kasi sana na sasa kampuny ilijulikana kimataifa..
Nilijua mimi kama Hance kwa uwezo nilionao ulitosha kabisa kuoa kwani nilikua na nyumba nzuri hata usafiri mzuri hivyo niliamua kuwapigia simu wazazi wangu waliokua wanaishi tanga vijijini na kiwapa wao jukumu la kunitafutia mke kwani nikiamini mabinti wengi mjini walinipenda kutokana na mali zangu
Nilipanga safari ya kwenda kijijini kwetu..niliamua kumuweka wazi rafiki yangu Said ambae alionesha kushangaa sana ni vipi msomi kama mimi kuamia kwenda kuoa kikijini lakini nilimjibu kua hata hao wa vijijini wanaitaji wasomi ili nao waelimike...
Kwakua tayari nilishapanga hakua na chakunishauri zaidi ya kunisindikiza kikijini kwetu...
Tukiwa tayari tumeshaanza vijiji vya mwanzo kuingia kikijini kwetu niloshangaa kidogo kuona kumwbadilika kwani nilipata tanu ya kujua wapi nipite hivyo nilikua naenda tu kwa kuotea
Gari yangu aina ya prado ikiwa taratibu inaendelea kupambana na matope ya njiani kwa mbali kwenye saitma niliona mwanamke aliejazia kwenye mahips anakuja akiwa pekupeku kavaa kanga huku kichwani kwake akiwa amebeba ndoo ya maji...
Bila kusita nilisimamisha gari kumsubiria nimuulize huku nikiendelea kumthaminisha kwenye kioo..
Samahana dada...nilimsimamisha na yeye akasimama kunisikiliza...
Salaam alykum...alinisalimia na mimi nikaitikia kisha nilauliza mahala alipokua anaishi mzee Kasukwa..
Mrembo yule alionesha kumfahamu mzee huyo hivyo alinielekeza kwa umaahili huku akionesha kwa vitendo lakini macho yangu yaliendelea kuduwaa huku nikishindwa kuamini kama kijijini pia kulikua kuna warembo kiasi hicho...
Hakuna anaejua ni vipi kiswahili chake cha kitanga kilivyokua kikiniua zaidi...
Nilijikuta nikitamani kumjua zaidi msichana yule mpaka hata baada ya kunielekeza silufanya makosa ya kuja kujilaumu baadae...niliamua kumuuliza jina na kuniambia anaitwa Memkido...nilitaka kujua maana ya jina hilo.lakini hata yeye hakujua maana yake..
Nilimuuliza wapi anaishi kwa aibu hulu akisugua mgiu wake chini alinielekeza nq hapo ndipo nilipomruhusu aende niliahidi kumtafuta...
Nilifika mapaka nyumbani na kupokewa kwa furaha na shangwe kwani ni miaka mingi sana sikurudi nyumbani tangu niondoke
Mama alijiambia ninawe miguu kwenye beseni kisha alikunuwa maji yale kwani aliweka nadhiri ya kufanya hivyo kama ningerud salama...
Muda wote huo Said hakua mwenye kuongea kwani alichukoa kabisa uaamuzi wangu wa kuoa kijijini..
Tukiwa tumeuzunguka mato usiku mimi na familia yangu huku mbuz akiwa kati kila mtu akikata kiasi alichohitaji niliamua kuanza kuelezea marengo makuu ya safari yangu huku mama akionesha kufurahia uamuzi wangu wa kuja kuoa nyumbani na kuniambia tayari binti yupo na wameshaongea na familia yake wamekubali kumuozesha binti yao kwangu...
Nilimsikiliza mama na baba kisha nikawaambia tayari yupo binti ninayetaka kumuoa hivyo huyo wakwao simhitaji..
Mama alishangaa ni kwanini sasa nilisema nataka kuo kijijini ikiwa tayari ninamwanamke wa kuoa kutoka mjini
Niliamua kueleza kuhusu msichana Memkido ambae nilimuona wakati nipo mjiani...
Wazazi wangu walipinga kabisa si kwasababu walimchukia msichana huyo ila walikua na ugomvi wa kifamilia kwani familia ya Memkido ilikua inaidai shilingi 30000 mpaka kufikia hatua ya kufikishana mahakamani..
Niliwaambia wazazi wangu kuwa hilo ni tatizo dogo lakini walipinga katukatu mimi kumuoa Memkido wakiamini familia y
ao iliizaririsha familia yetu....
Itaendelea....

0 maoni:
Post a Comment
to maoni n ushauri wako kuhusu post zetu