Slider

Ephonix Music Tz

Rich Mavoko Na Skendo Ya Kutumia Mkorogo, Isome Hapa


   
BONGO Fleva inazidi kupaa na kupata hadhi
ya kuwa ndiyo muziki wa Afrika Mashariki
katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda,
Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Kongo (DRC). Kutoka enzi za Kwanza Unit hadi uzao wa
akina Ruby, ni safari ndefu iliyozalisha
wasanii wengi waliofanya vizuri na kutoa
mchango wao katika kiwango cha kuridhisha.
Na kati yao, ni kijana Rich Movoko ambaye
kwa mashabiki wa muziki huu, ni jina kubwa
lenye hadhi. Ni kizazi cha Bongo Fleva kilichoibuka ‘enzi’
moja na akina Diamond Platnumz, yapata
miaka saba au nane iliyopita. Sijawahi kuwa
karibu na huyu dogo, lakini nikiri kuwa kazi
zake nazisikia na zinafanya vizuri, hasa kibao
chake cha hivi karibuni zaidi kiitwacho Pacha
Wangu. Kama utataka kuwaweka katika chati,
utakutana na Rich Mavoko katika nafasi za
juu akishindana na kina Ali Kiba, Diamond,
Barnaba, Madee na wenzake wa namna hiyo.
Ni mzuri na kwa kweli ana heshima yake
katika muziki huu.
Lakini kuna jambo moja limekuwa likinitatiza
kidogo kumhusu, hasa katika maisha yake
binafsi. Labda kabla sijaenda mbali,
niwakumbushe mastaa kuwa ukishakuwa mtu
maarufu, suala la ‘privesi’ linaondoka. Ni
vigumu kumkuta Mavoko anakula wali
maharage kwa mama ntilie, ule wa buku jero,
halafu useme hilo ni jambo binafsi!
Hiyo itakuwa ni habari kubwa, ingawa kuna
watu wana hela kuliko yeye wanakula hapo,
lakini kwa kuwa hawajulikani, hakuna
anayejali.
Rich Mavoko inadaiwa anatumia mkorogo.
Wakati anaibuka, hata yeye anajua kuwa
alikuwa mweusi, lakini ukionana naye hivi
sasa, ni mweupe. Wakati f’lani aliwahi
kuwajibu wanaomsema kuhusu mkorogo,
akisema kuwa hatumii madawa, isipokuwa
labda tu kwa vile hali yake kimaisha ni nzuri,
ndiyo maana na ngozi nayo inakuwa safi!
Utetezi dhaifu kabisa. Kwamba kwa kuwa mambo yake yako vizuri,
basi na ngozi nayo inabadilika rangi? Big no!
Hakuna uhusiano kati ya fedha na rangi ya
ngozi bila kujichubua. Alifanya hivyo Michael
Jackson na dunia yote inajua, jinsi
alivyoichukia ngozi yake nyeusi. Kama suala ni hela, pale katika Ligi Kuu
England kuna Mbrazil anaitwa Ramires,
anakipiga Chelsea. Ana hela na kule anaishi
sehemu wanazoishi wenye nazo, lakini kama
utamchukua na kumtupa pale shimoni, sokoni
Kariakoo na ukaambiwa jamaa anatokea
Masasi, hakuna atakayehoji. Mavoko anadaiwa kutumia cosmetics kali
kama siyo mkorogo kujichubua. Naweza
kusema hayo ni maisha yake binafsi, lakini
kama nilivyosema, ukiwa staa, lolote
litafuatiliwa. Kuna watoto wetu wanaangalia
televisheni, walimuona akiwa mweusi, ghafla
leo kawa ‘white’, watajiuliza na wakisikia
kuna mchanganyiko wa madawa yanabadili
rangi ya ngozi, wanaweza kushawishika. Nimshauri mdogo wangu Rich Mavoko, kuwa
international siyo kubadili rangi ya ngozi
yako, ufanane na Mzungu. Fanya kazi nzuri
na tengeneza menejimenti ya uhakika,
utakuwa msanii wa kimataifa. AY amefanya muziki kabla yake, amekuwa
international kabla yake na ameshafanya
kolabo kibao na mastaa wa Marekani, lakini
kila siku rangi yake ya ngozi ni ileile, tena
inazidi kuiva kiuweusi. Madoido ya wasanii, hasa wa Bongo ni
jambo la kawaida, lakini yasifikie wakati watu
wakakuona limbukeni au uliyeathiriwa na
ustaa. Tunao mastaa, ambao walidhani wao
ni wajanja, wakaiga ujinga, leo ulimwengu
unawacheka, wamepoteza hata kile kidogo
walichokuwa nacho. Mavoko bado kijana, kama kweli unatumia
mkorogo kama inavyodaiwa achana nao,
mashabiki wanataka kazi bomba na wala
hawana haja na muonekano wako !
-GPL
Share on Google Plus

About Chill Axy Beatz

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment

to maoni n ushauri wako kuhusu post zetu