Sakata
la kusambaa picha zisizokuwa na maadili mitandaoni zikiwemo za watu
maarufu hapa nchini leo limezungumziwa tena katika bunge la Tanzania
kule Dodoma ambapo katika kipindi cha maswali na majibu Mhe. Habib Mnyaa
ameonekana akihoji serikali inachukua hatua gani juu ya watu wanaotuma
picha zao zisizo na maadili mitandani zikiwemo za kina Wema na Diamond
wanazopiga wakiwa chumbani...
Katika majibu yake waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia Prof. Makame Mbarawa anasema
“Mhe.
Spika kuhusu picha zisizokuwa na maadili zinazowekwa katika mitandao na
watu maarufu na hata wasiokuwa maarufu serikali imeanza kuandaa kanuni
zitakazokuwa zikifuatilia Online Content ambapo itaanza kuchukua hatua
baada ya kufuatilia juu ya picha hizo na kuchukua hatua madhubuti”.
Baada ya kauli
hiyo Spika wa bunge Mhe. Anne Makinda alikazia akitaka majibu juu ya
picha za juzi zilizosambaa zikimuonyesha Mhe. Komba akiwa na binti mdogo
ambazo mwenyewe alisema si zake na wabunge kuonekana wakitaka majibu
ambapo Mhe. Mbarawa anasema.
“Mhe. Spika
kuhusu picha za juzi zilizosambaa mitandaoni tunazifuatilia kujua
zimeanzia wapi na taarifa zake zikoje kwani hata mimi bado sijaziona ila
tutachukua hatua tutakapobaini zilipotoka.”
0 maoni:
Post a Comment
to maoni n ushauri wako kuhusu post zetu