
Wasaniii
walioshiriki tamasha la Fiesta 2014 wakiwa na mishumaa jukwaani
wakisambaza upendo na kuwafariji wale wote waliopotelewa na ndugu
zao,waliojeruhiwa katika ajali iliyotokea hivi karibuni wilayani
Butiama mkoani Mara,ambapo watu zaidi ya 40 walipoteza maisha na wengine
kujeruhiwa vibaya.
Ulifika wakati wa kutoa pale na kusambaza upendo kwa wakazi wa Mji wa Musoma na Vitongoji vyake,kufuatia ajali mbaya ya mabasi mawili yaliyogongana uso kwa uso na kupoteza maisha ya zaidi 40.
Mmoja wa wasanii anaekuja juu katika anga ya muziki wa hip hop,Young Killer a.k.a Msodoki akiwaimbisha mashabiki wake jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja wa Kaume.
Mmoja
wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Barnaba ambaye kwa sasa
anatamba na wimbo wake mpya ujulikanao kwa jina la Waharade akiwaimbisha
wakazi wa mji wa musoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la fiesta 2014
Mwanadada machachari awapo jukwaani,Shilole akiimba kwa madaha kabisa kwenye jukwaa la Fiesta ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Mmoja
wa wanamuziki mahiri ,Christian Bella ambaye kwa sasa anatamba na
wimbo wake wa nani kama Mama,akiwaimbisha wakazi wa musoma
waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta usiku huu.
Wasanii
wa Kundi la Wanaume TMK,a.k.a Wakata Mkaa Themba na Chege
wakilishambulia jukwaa la fiesta lililofanyika katika uwanja wa Karume,mjini Musoma ambao maelfu ya watu walijitokeza kulishuhudia tamasha hilo.
Msanii
wa hip hop katika miondoko ya Bongofleva atambulikae kwa jina la
kisanii Roma,akitumbuiza jukwaani mbele ya umati wa wakazi wa mjini
Musoma kwenye tamasha la fiesta 2014 ndani ya uwanja wa Karume.
Wakali
wa hip hop,Ney wa Mitego na Stamina wakilishambulia jukwaa kwa pamoja
kwa wimbo wao uitwao huko kwenu vipi,huku miluzi na shangwe za
mashabiki zikiwa zimetawala uwanjani hapo.
.jpg)

.jpg)

.jpg)

.jpg)















0 maoni:
Post a Comment
to maoni n ushauri wako kuhusu post zetu